Wednesday, 26 August 2026

NDEJEMBI AWABANA WAKANDARASI WAZEMBE

Waziri wa Nishati, Dk. Deogratius Ndejembi, ameagiza wakandarasi wanaosuasua na wenye historia ya kuchelewesha utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini kutopatiwa kazi mpya, huku akizitaka taasisi husika kuzipa kipaumbele kampuni zinazotekeleza miradi kwa ufanisi na kukamilisha kazi kwa wakati. Dk. Ndejembi ametoa maelekezo hayo Juni 22, 2026 wakati akifungua mkutano wa tathmini ya utekelezaji […]

Waziri wa Nishati, Dk. Deogratius Ndejembi, ameagiza wakandarasi wanaosuasua na wenye historia ya kuchelewesha utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini kutopatiwa kazi mpya, huku akizitaka taasisi husika kuzipa kipaumbele kampuni zinazotekeleza miradi kwa ufanisi na kukamilisha kazi kwa wakati.

Dk. Ndejembi ametoa maelekezo hayo Juni 22, 2026 wakati akifungua mkutano wa tathmini ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini uliowakutanisha viongozi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakandarasi na wadau mbalimbali wa sekta ya nishati jijini Dar es Salaam.

Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha uwajibikaji, kuongeza ushindani wenye tija miongoni mwa wakandarasi na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ili wananchi wengi zaidi waweze kupata huduma ya umeme kwa wakati.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia viwango vya ubora katika utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha uwekezaji unaofanywa na Serikali unaleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *