Wednesday, 26 August 2026

MWANAFUNZI DARASA LA TATU AUAWA MTWARA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limethibitisha kifo cha mwanafunzi wa darasa la tatu, Moreen Nyamajeje (9), mkazi wa Mtaa wa Lilungu Manispaa ya Mtwara Mikindani, ambaye inadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na watu wasiojulikana. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ASCP Issa Suleiman, amesema tukio hilo lilitokea jioni ya Juni 21, 2026, baada ya mtoto […]

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limethibitisha kifo cha mwanafunzi wa darasa la tatu, Moreen Nyamajeje (9), mkazi wa Mtaa wa Lilungu Manispaa ya Mtwara Mikindani, ambaye inadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ASCP Issa Suleiman, amesema tukio hilo lilitokea jioni ya Juni 21, 2026, baada ya mtoto huyo kuchukuliwa na watu wasiojulikana kabla ya mwili wake kupatikana ukiwa hauna uhai.

Kwa mujibu wa Kamanda Suleiman, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira, chanzo cha tukio hilo pamoja na kuwabaini na kuwakamata waliohusika na mauaji hayo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Zawadi Bwanali, amethibitisha kupokea mwili wa mtoto huyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu ili kubaini chanzo halisi cha kifo chake.

Kutokana na tukio hilo Polisi wametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia uchunguzi na kufanikisha kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *