‎Msanii maarufu wa muziki kutoka Tanzania, Rayvanny, ametangaza kwa furaha ushiriki wake katika matukio yanayohusiana na Kombe la Dunia la FIFA 2026 yatakayofanyika jijini Toronto nchini Canada tarehe 10 Juni 2026.

‎Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny alieleza kuwa ndoto kubwa zinaweza kutimia, akionesha furaha yake ya kuwa sehemu ya matukio ya kuelekea mashindano ya FIFA World Cup 2026.

‎Aidha Msanii huyo alitumia ujumbe wa hamasa akisema kuwa dunia nzima itaunganishwa kupitia muziki na soka katika tukio hilo kubwa la kimataifa.

‎Taarifa hilo imepokelewa kwa shangwe na mashabiki wake pamoja na wadau wa burudani, ambao wameeleza kuwa ushiriki wa Rayvanny katika jukwaa la Kombe la Dunia ni hatua nyingine kubwa inayodhihirisha ukuaji wa muziki wa Tanzania katika soko la kimataifa.

‎Kombe la Dunia la FIFA 2026 linatarajiwa kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya michezo duniani, likifanyika katika nchi za Canada, United States na Mexico.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here