GUEYE AINGIA ANGA ZA MUSONDA, INONGA

Date:

Share post:

BAO la dakika ya tatu alilofunga Libasse Gueye katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Yanga limemfanya mshambuliaji huyo wa Simba kufuata nyayo za mastaa wa zamani wa timu hizo, Kennedy Musonda na Enock Innonga.

Gueye raia wa Senegal, anaungana nao katika orodha ya wachezaji watatu waliofunga mabao ya mapema zaidi katika ‘Kariakoo derby’ 10 zilizopita za Ligi Kuu Bara.

Kama ilivyo kwake, Musonda akiwa na Yanga aliitungua Simba katika dakika ya tatu, mchezo uliochezwa Novemba 5, 2023 na Simba kupoteza kwa kichapo cha mabao 5-1.

Mabao mengine ya Yanga katika mechi hiyo yalifungwa na Maxi Nzengeli (mawili), Pacome Zouzoua na Stephanie Aziz Ki, huku Simba wakipata bao kupitia kwa Kibu Dennis.

Kwa upande wa Inonga, bado ndiye mchezaji mwenye rekodi ya bao la mapema zaidi katika derby za miaka ya hivi karibuni, akiwapiku Musonda na Gueye.

Beki wa kati huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), aliifunga Yanga katika dakika ya kwanza ya derby iliyochezwa Aprili 16, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe, ni mchezo ambao Simba wakiwa wenyeji walizoa pointi zote tatu, bao lao jingine likifungwa na Kibu katika dakika ya 32.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KISWAHILI KUIMARISHWA NCHINI KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha matumizi ya Kiswahili...

‘KARIAKOO DERBY’ YAVUNJA REKODI YA MABAO

BAADA ya sare ya mabao 2-2 jana Mei 3, 2026, mechi inayozikutanisha Simba na Yanga, maarufu kwa jina...

MASTAA WA KIGENI WAENDELEA KUTAMBA ‘KARIAKOO DERBY’

DAKIKA 90 za 'Kariakoo Derby' zilitamatika jana Mei 3, 2026 katika Uwanja wa Jenerali Isamhuyo jijini Dar es...

PANYA, NGUCHIRO WANAVYOTESA RAIA WA PALESTINA UKANDA WA GAZA

JERUSALEM, Palestina NI katika kambi za raia wa Palestina wanaoishi kwenye mahema baada ya makazi yao kusambaratishwa na mashambulizi...