Saturday, 10 October 2026

VIJANA ARUSHA WAHIMIZWA KUEPUKA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Arusha amewataka vijana wa Mtaa wa Bondeni, Kata ya Kati jijini Arusha kujiepusha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kufuata taratibu za kisheria wanapokabiliana na changamoto mbalimbali za kiusalama katika maeneo yao. Akitoa elimu ya usalama kwa vijana hao leo Juni 5, 2026, amesema kuwa utunzaji […]

Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Arusha amewataka vijana wa Mtaa wa Bondeni, Kata ya Kati jijini Arusha kujiepusha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kufuata taratibu za kisheria wanapokabiliana na changamoto mbalimbali za kiusalama katika maeneo yao.

Akitoa elimu ya usalama kwa vijana hao leo Juni 5, 2026, amesema kuwa utunzaji wa amani na usalama ni jukumu la kila mwananchi na unahitaji ushirikiano wa karibu kati ya jamii na vyombo vya dola pamoja na utii wa sheria bila shuruti.

Amesema kufuata misingi ya sheria husaidia kuimarisha utulivu, mshikamano na maendeleo ya jamii, huku akionya kuwa vitendo vya kujichukulia sheria mkononi vinaweza kusababisha madhara makubwa na kuvuruga amani iliyopo.

Aidha, amewahimiza vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za ulinzi shirikishi kwa kuunda vikundi vitakavyosaidia kuzuia uhalifu na kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na Jeshi la Polisi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *