Sunday, 11 October 2026

MENEJIMENTI YA WIZARA YA UJENZI YAJENGEWA UELEWA WA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi imepata elimu kuhusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira katika utekelezaji wa miradi ya barabara, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha maendeleo ya sekta ya ujenzi yanaendana na misingi ya utunzaji wa mazingira. Elimu hiyo ilitolewa leo Juni 4, 2026, wakati Menejimenti hiyo ilipotembelea banda la Wizara ya Ujenzi pamoja […]

Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi imepata elimu kuhusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira katika utekelezaji wa miradi ya barabara, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha maendeleo ya sekta ya ujenzi yanaendana na misingi ya utunzaji wa mazingira.

Elimu hiyo ilitolewa leo Juni 4, 2026, wakati Menejimenti hiyo ilipotembelea banda la Wizara ya Ujenzi pamoja na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) katika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma, ambako yanaendelea Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026.

Kupitia ziara hiyo, viongozi hao walipata fursa ya kujifunza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na sekta ya ujenzi katika kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa na kulindwa wakati wa utekelezaji wa miradi ya barabara nchini.

Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na TANROADS inashiriki katika maonesho hayo kwa lengo la kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa maendeleo endelevu ya taifa.

Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2026 kinatarajiwa kufanyika kesho, Juni 5, 2026, yakiongozwa na kaulimbiu isemayo, “Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *