Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza kuwa limekusanya kundi la wasanii mashuhuri wa muziki kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwa ajili ya Albamu Rasmi ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.

‎ Kwa mujibu wa Rais wa FIFA, Gianni Infantino, ameeleza albamu hiyo itawakutanisha mastaa wa kimataifa pamoja na vipaji vinavyoibukia, kwa lengo la kuleta umoja miongoni mwa mashabiki wa soka kupitia muziki.

‎Pia albamu inatarajiwa kuwa na nyimbo kutoka kwa wasanii wa lugha, tamaduni na mitindo tofauti ya muziki, ikionyesha utofauti wa dunia na roho ya mshikamano inayobebwa na FIFA World Cup 2026.

‎ FIFA inaamini kuwa muziki, kama ilivyo soka, una uwezo mkubwa wa kuwaleta watu pamoja bila kujali tofauti zao.

‎Hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Dunia 2026, yanayotarajiwa kuvutia mamilioni ya mashabiki duniani kote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here