Mchezaji wa RB Leipzig, Yan Diomandé, ameibua mjadala kuhusu hatma yake baada ya kueleza wazi mapenzi yake kwa Paris Saint-Germain wakati akihusishwa na uhamisho wake majira ya joto.
Diomandé amesema amekuwa akiipenda PSG tangu akiwa mtoto kutokana na ushawishi wa baba yake ambaye ni shabiki wa klabu hiyo.
Aidha, amesisitiza kuwa angefurahia kupata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho cha mabingwa wa Ufaransa.
Ripoti zinaeleza kuwa PSG na Liverpool FC zote zinafanya mazungumzo ya kumsajili nyota huyo kutoka RB Leipzig katika dirisha la usajili la majira ya joto.
Licha ya kuhusishwa na klabu hizo mbili kubwa, Diomandé amesema kwa sasa akili yake yote imeelekezwa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia, huku akiacha maamuzi ya usajili yashughulikiwe na klabu husika baada ya mashindano hayo kumalizika.
Kauli yake imeongeza uwezekano wa PSG kuwa na nafasi kubwa ya kumpata mchezaji huyo, ingawa Liverpool nayo inaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya mazungumzo hayo.
DIOMANDE AFUNGUKA KUHUSU PSG HUKU LIVERPOOL WAKIMTAKA
Mchezaji wa RB Leipzig, Yan Diomandé, ameibua mjadala kuhusu hatma yake baada ya kueleza wazi mapenzi yake kwa Paris Saint-Germain wakati akihusishwa na uhamisho wake majira ya joto.Diomandé amesema amekuwa akiipenda PSG tangu akiwa mtoto kutokana na ushawishi wa baba yake ambaye ni shabiki wa klabu hiyo.Aidha, amesisitiza kuwa angefurahia kupata nafasi ya kucheza katika […]
