Mgombea urais wa klabu ya Real Madrid, Enrique Riquelme, ameibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki baada ya kutangaza kuwa kiungo nyota wa Hispania, Rodri, ndiye atakuwa usajili wake mkuu endapo atashinda uchaguzi wa kuiongoza klabu hiyo.
Riquelme amesema ana dhamira ya kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha Rodri anajiunga na Real Madrid, akiamini kuwa nyota huyo anaweza kuongeza nguvu kubwa katika kikosi cha mabingwa hao wa Ulaya.
Mbali na hilo, mgombea huyo ameahidi pia kumleta kocha mwenye hadhi kubwa duniani ambaye anadaiwa kupendwa na mashabiki wa Real Madrid.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa kocha huyo si José Mourinho, jambo ambalo limezua maswali mengi kuhusu jina analolenga kulitangaza siku zijazo.
Kauli za Riquelme zimeongeza hamasa kuelekea uchaguzi wa uongozi wa Real Madrid, huku mashabiki wakisubiri kuona iwapo ahadi hizo zitatekelezeka endapo atapata nafasi ya kuiongoza klabu hiyo.
Home MICHEZO Michezo Kimataifa MGOMBEA URAIS REAL MADRID AAHIDI KUMSAJILI RODRI NA KUMLETA KOCHA WA VIWANGO







