Sunday, 11 October 2026

TRUMP KUHUDHURIA MKUTANO WA G7 NCHINI UFARANSA

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa atahudhuria mkutano wa viongozi wa mataifa tajiri ya G7 utakaofanyika nchini Ufaransa kuanzia Juni 15 hadi 17 mwaka huu. Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wake wa Truth Social siku ya Jumatano, Trump alisema atasafiri kuelekea Ufaransa mara baada ya tamasha la mapigano ya sanaa za kijeshi (UFC) litakalofanyika […]

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa atahudhuria mkutano wa viongozi wa mataifa tajiri ya G7 utakaofanyika nchini Ufaransa kuanzia Juni 15 hadi 17 mwaka huu.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wake wa Truth Social siku ya Jumatano, Trump alisema atasafiri kuelekea Ufaransa mara baada ya tamasha la mapigano ya sanaa za kijeshi (UFC) litakalofanyika katika Ikulu ya Marekani (White House) kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya miaka 80 tarehe 14 Juni.

Kundi la G7 linaundwa na mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi duniani ambayo ni Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Canada na Japan, pamoja na Umoja wa Ulaya.

Mkutano huo wa kilele unatarajiwa kujadili masuala mbalimbali ya kimataifa yakiwemo uchumi, biashara, usalama na changamoto za kisiasa zinazoikabili dunia kwa sasa.

Mwaka uliopita, Canada ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa G7 uliowakutanisha viongozi wa nchi wanachama kujadili masuala muhimu yanayoathiri uchumi na ushirikiano wa kimataifa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *