Sunday, 23 August 2026

RUBIO AONYA HATARI YA VITA KUONGEZEKA KATI YA URUSI NA UKRAINE

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ameonya kuhusu hatari kubwa ya kuongezeka kwa mvutano katika vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine, akieleza kuwa hali ya sasa inaweza kusababisha mzozo huo kuwa mkali zaidi. Akizungumza mbele ya kamati ya Bunge la Marekani, Rubio alisema hatari hizo zimeongezeka kutokana na uwezo unaoongezeka wa […]

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ameonya kuhusu hatari kubwa ya kuongezeka kwa mvutano katika vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine, akieleza kuwa hali ya sasa inaweza kusababisha mzozo huo kuwa mkali zaidi.

Akizungumza mbele ya kamati ya Bunge la Marekani, Rubio alisema hatari hizo zimeongezeka kutokana na uwezo unaoongezeka wa Ukraine kufanya mashambulizi ndani kabisa ya eneo la Urusi, jambo ambalo linaweza kuzidisha mapambano kati ya pande hizo mbili.

Rubio alisisitiza kuwa Marekani iko tayari kushiriki katika juhudi zozote zitakazosaidia kufanikisha amani na kumaliza vita hivyo. Alieleza kuwa Washington inaamini hakuna suluhisho la kijeshi kwa mzozo huo, bali njia ya mazungumzo ndiyo inaweza kuleta suluhu ya kudumu.

Hata hivyo, alisema bado hakuna dalili za pande zote mbili kuwa tayari kufanya makubaliano yatakayowezesha kusitishwa kwa vita, hali inayofanya matumaini ya amani ya haraka kuwa finyu.

Aidha, Rubio alikiri kuwa Marekani haiwezi kujitambulisha kama mpatanishi huru katika mzozo huo kwa sababu inaendelea kuipatia Ukraine silaha za kijeshi na wakati huohuo kudumisha vikwazo mbalimbali dhidi ya Urusi ambapo Kauli hiyo imekuja wakati juhudi za kimataifa za kutafuta suluhu ya vita hivyo zikiendelea kuongezeka.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *