Monday, 24 August 2026

SABA WAFARIKI DUNIA 17 WAKIJERUHIWA KATIKA AJALI SINGIDA

Watu saba wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Senkenke, wilayani Iramba mkoani Singida, baada ya lori kupata hitilafu ya mfumo wa breki na kugonga nyuma basi dogo aina ya Coaster. Ajali hiyo imetokea leo Juni 2, 2026 majira ya saa 4:00 asubuhi wakati lori hilo lililokuwa likishuka […]

Watu saba wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Senkenke, wilayani Iramba mkoani Singida, baada ya lori kupata hitilafu ya mfumo wa breki na kugonga nyuma basi dogo aina ya Coaster.

Ajali hiyo imetokea leo Juni 2, 2026 majira ya saa 4:00 asubuhi wakati lori hilo lililokuwa likishuka mlima Senkenke lilipogongana na Coaster lililokuwa likitoka Singida kuelekea Igunga mkoani Tabora, kabla ya magari yote mawili kutumbukia kwenye korongo kando ya barabara kuu ya Dar es Salaam–Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amefika eneo la tukio na baadaye kuwatembelea majeruhi waliolazwa hospitalini na kutoa pole kwa familia zilizoathirika. Pia ameagiza uchunguzi wa kina wa chanzo cha ajali hiyo.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Peter Luhega, amesema majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu huku baadhi yao wakiwa katika hali ya uangalizi maalumu kutokana na majeraha waliyopata.

Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo na miili ya marehemu imehifadhiwa kwa ajili ya utambuzi na taratibu nyingine za mazishi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *