Timu ya taifa ya Mali, maarufu kama Les Aigles du Mali (Tai wa Mali), imeanza rasmi maandalizi yake kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Iran utakaochezwa tarehe 4 Juni mjini Antalya, nchini uturuki.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ukurasa rasmi wa timu hiyo, wachezaji wa Mali walifanya kikao chao cha kwanza cha mazoezi alasiri huko Antalya.
Mazoezi hayo yalifanyika katika uwanja wa Gloria Sports Arena Complex, ambapo jumla ya wachezaji 20 walihudhuria na kushiriki kikamilifu.
Aidha chezo huo wa kirafiki dhidi ya Iran ni sehemu ya maandalizi ya timu ya Mali kwa mashindano na mechi zijazo za kimataifa.
Kwa upande wa Benchi la ufundi hilo linatarajia kutumia mechi hiyo kupima uwezo wa kikosi na kuimarisha mbinu mbalimbali kabla ya ratiba nyingine muhimu.
Home MICHEZO Michezo Kimataifa TIMU YA TAIFA YA MALI YAANZA MAANDALIZI YA MCHEZO WA KIRAFIKI DHIDI...







