SAMIA ATEUA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 20, 2026 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu uteuzi huo ni wa majaji tisa kutoka Mahakama Kuu Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Walioteuliwa ni Abdi Shaaban Kagomba, Yohane Masara, Immaculata Banzi, Rabia Mohamed, Cyprian Mkeha, Yose Mlyambina, Imani Aboud, Mzee Ibrahim pamoja na Juliana Masabo.

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, uapisho wa majaji hao wa Mahakama ya Rufani utafanyika tarehe itakayopangwa hapo baadaye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here