SERIKALI KUENDELEA KUNUNUA MELI MPYA NA KUKARABATI ZILIZOPO – PROF. MAKAME MBARAWA

Date:

Share post:

WAZIRI wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Serikali kupitia TASHIKO imeendelea kusimamia ununuzi wa meli mpya, pamoja na ukarabati wa meli zilizopo ili kuimarisha usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo.

Kwa kipindi cha Julai, 2025, hadi Machi, 2026, TASHICO ilisafirisha abiria 128, 191 na tani za mzigo 71,796.25, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 22.51, ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, wakati wa uwasilishaji wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026-27 Bungeni jijiji Dodoma.

Katika hotuba yake, Waziri Mbarawa amesema Serikali imekamilisha ujenzi wa meli ya MV Mwanza katika Ziwa Victoria.

“Pia, Serikali imendelea na ukarabati wa meli zingine katika Ziwa Victoria, ambapo ukarabati wa meli ya MV Ukerewe umefikia asilimia 79.

“Vilevile, Serikali kupitia Kampuni ya Meli nchini (TASHICO) imeanza ujenzi wa meli ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,000 za mizigo katika Ziwa hilo,” amesema.

Vilevile, kutokana na umuhimu wa Ziwa Tanganyika, Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwamo ujenzi wa meli nne za mizigo zilizojengwa na TPA kwa kushirikiana na sekta binafsi, ambazo zimekamilika na kila moja ina uwezo wa kubeba tani 2,000 za mizigo.

Akieleza miradi ya kimkakati iliyopo, Waziri Mbarawa amesema kuna ujenzi wa meli mpya ya abiria, sambamba na ujenzi wa karakana ya ujenzi wa meli.

“Nne, kuanza ujenzi wa magati mawili ya kisasa katika Bandari ya Kigoma, ambayo hadi kufikia mwezi Machi, 2026, utekelezaji wake umefikia asilimia 13.

“Tano, ni kuendelea na ukarabati wa meli ya MV Liemba, ambapo ukarabati wake umefikia asilimia 64,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI ZA SITISHWA KATIKA MITO YA MTISI NA IBANDA MKOANI KATAVI

Serikali imechukua hatua kali dhidi ya ukiukwaji wa sheria katika sekta ya madini baada ya Waziri wa Madini,...

MLANGO-BAHARI WA HORMUZ UNAVYOITESA DUNIA

TEHRAN, Iran MGOGORO unaoendelea kati ya Iran na Marekani katika Mlango-Bahari wa Hormuz umetikisa uchumi wa dunia. Kila nchi,...

MWAKA MMOJA WA PAPA LEO AKIIONGOZA VATICAN

WASHINGTON DC, Marekani UMETIMIA mwaka mmoja tangu Papa Leo XIV alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki duniani. Aliingia madarakani Mei 8,...

STEVE BARKER AMEANZA KUJIPATA LIGI KUU BARA

UKIFUATILIA msimamo wa Ligi Kuu Bara na kiwango cha Simba katika mechi za hivi karibuni, unaweza kusema sasa...