Sunday, 11 October 2026

CUBA YALAANI VIKWAZO VIPYA VYA MAREKANI

HAVANA, CubaWAZIRI wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bruno Rodriguez, ameviita kuwa ni ukatili vikwazo vipya walivyowekewa na Marekani. Jana Mei Mosi, 2026, Rais Donald Trump alisaini agizo la vikwazo vipya kwa viongozi wa sekta za nishati, ulinzi, fedha na ulinzi nchini Cuba. Pia, vikwazo hivyo vimekumba baadhi ya viongozi waliotajwa na Marekani kujihusisha na […]

HAVANA, Cuba
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bruno Rodriguez, ameviita kuwa ni ukatili vikwazo vipya walivyowekewa na Marekani.

Jana Mei Mosi, 2026, Rais Donald Trump alisaini agizo la vikwazo vipya kwa viongozi wa sekta za nishati, ulinzi, fedha na ulinzi nchini Cuba.

Pia, vikwazo hivyo vimekumba baadhi ya viongozi waliotajwa na Marekani kujihusisha na vitendo vya rushwa na ukikwaji wa haki za binadamu.

Maagizo hayo yanakuja baada ya maandamano ya wafanyakazi nchini Cuba kufika nje ya ofisi za Ubalozi wa Marekani.

Hoja ya maandamano hayo ni kukosoa hatua ya Marekani kuzuia nishati ya mafuta kuingia Cuba, hali inayoathiri uchumi wa Taifa hilo na kupanda kwa gharama za maisha.

Kwa upande mwingine, Rais Trump amenukuliwa mara kadhaa akisema nia yake ni kuiondosha madarakani Serikali ya kijamaa inayokiongoza Kisiwa hicho.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *