KAMBI YA WAKIMBIZI NDUTA KUFUNGWA KUFUATIA UREJESHWAJI WA HIARI WA WAKIMBIZI BURUNDI

Date:

Share post:

Kambi ya Wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma inatarajiwa kufungwa rasmi Leo Aprili 30, 2026, kufuatia utekelezaji wa mpango wa kurejesha wakimbizi wa Burundi kwa hiari nchini kwao.

Baada ya kufungwa kwa kambi hiyo, miundombinu ya huduma ikiwemo majengo ya kudumu pamoja na vitendea kazi vingine itakabidhiwa kwa Serikali kwa ajili ya kuandaliwa matumizi mengine ya eneo husika.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa 26 wa pande tatu kati ya Serikali ya Tanzania, Serikali ya Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), uliofanyika Novemba 2025 jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, ilikubaliwa mpango wa kufungwa kwa kambi ya Nduta ifikapo Machi 31, 2026, lakini baadaye muda huo uliongezwa hadi Aprili 30, 2026 kutokana na ombi la Serikali ya Burundi.

Aidha, mpango kazi huo unaeleza kuwa urejeshwaji wa wakimbizi wa Burundi waliopo katika Kambi ya Nyarugusu, Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma, utakamilika ifikapo Juni 30, 2026, hatua itakayofuatiwa na kufungwa kwa kambi hiyo pia.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, tayari amewasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, ambapo anatarajiwa kushuhudia na kuongoza ufungaji rasmi wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS DKT. MWINYI APOKEA RIPOTI YA CAG ZANZIBAR YA MWAKA 2024/2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameipokea Ripoti ya Mdhibiti...

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUENDELEZA USHIRIKIANO NA IRELAND

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar itaendelea kuimarisha...

INTANETI YA KASI YAFIKIA ASILIMIA 94 MAENEO YA MAKAZI WATUMIAJI WAKIFIKA ASILIMIA 85.3

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesema huduma ya intaneti ya kasi imefikia asilimia 94...

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUTOA ELIMU YA UPANDAJI MITI KWA BIASHARA YA KABONI

Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha...