WALIMU WA SAYANSI NA HISABATI WASHAURIWA KUWA WABUNIFU KUONGEZA UELEWA WA WANAFUNZI

Date:

Share post:

Walimu wanaofundisha masomo ya Sayansi na Hisabati nchini, wametakiwa kutumia teknolojia pamoja na mbinu bunifu za ufundishaji ili kuongeza uelewa kwa wanafunzi na kusaidia kuzalisha wataalamu wa sayansi watakaochangia maendeleo ya taifa kijamii na kiuchumi.

Wito huo umetolewa Aprili 29, 2026 na Ofisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Samson Allute, wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa walimu wa Sayansi na Hisabati kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Allute amesema matumizi ya teknolojia katika ufundishaji yatawawezesha walimu kufundisha kwa ufanisi zaidi huku yakichochea wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi na Hisabati tangu wakiwa mashuleni.

Amesema serikali inaendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP), unaolenga kuboresha miundombinu ya shule, kutoa mafunzo kazini kwa walimu pamoja na kuimarisha matumizi ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

“Mwalimu anapaswa kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri, kufanya ubunifu na kuwa wataalamu watakaosaidia maendeleo ya taifa,” amesema Allute.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea walimu uwezo wa kutumia teknolojia na mbinu shirikishi za ufundishaji ili kuboresha ufaulu wa wanafunzi katika masomo ya Sayansi na Hisabati.

Aidha, amewataka walimu kutumia maarifa watakayoyapata kuwasaidia wanafunzi kuondoa hofu ya masomo ya sayansi ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakionekana kuwa magumu kwa baadhi yao.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Happiness Goyi, mwalimu wa Kemia kutoka Shule ya Sekondari Mwakibuga mkoani Simiyu, amesema mafunzo hayo yatamsaidia kutumia mbinu za kisasa zitakazowawezesha wanafunzi kuelewa kwa urahisi masomo ya sayansi na kuyapenda zaidi.

Naye Daniel David, mwalimu wa Fizikia, amesema matumizi ya teknolojia katika ufundishaji yatawasaidia wanafunzi kuendana na mabadiliko ya dunia ya sasa yenye ushindani mkubwa wa sayansi na teknolojia.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwajengea uwezo walimu 523 kutoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Tabora na Katavi kupitia mradi wa SEQUIP.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SERIKALI YAIMARISHA USAMBAZAJI WA CHANJO IKIZINDUA BOTI 7 ZA BILION1.1

Serikali imeendelea kuimarisha huduma za chanjo nchini kupitia uzinduzi wa boti saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.1...

VYOMBO VYA HABARI NCHINI VYA TAJWA KUWA NGUZO YA KULINDA MAADILI YA MTANZANIA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali inavitegemea kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari...

RAIS DKT. MWINYI AKABIDHI KOMBE LA MUUNGANO 2026 KWA BINGWA SIMBA SPORTS CLUB

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaongoza maelfu ya mashabiki...

HANDENI KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA KUPITIA UGAWAJI WA VYANDARUA BURE

Katika kuendeleza jitihada za kupambana na ugonjwa wa malaria nchini, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa kushirikiana na...