HANDENI KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA KUPITIA UGAWAJI WA VYANDARUA BURE

Date:

Share post:

Katika kuendeleza jitihada za kupambana na ugonjwa wa malaria nchini, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imefanya mkutano maalumu kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Ugawaji wa Vyandarua Ngazi ya familia bila malipo.

Mkutano huo umefanyika leo Aprili 29, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa hospitali ya Halmashauri, ukihusisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakiwemo wataalamu, watendaji wa serikali na viongozi wa dini.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Ndg. Saitoti Stephen, amesema kuwa ugawaji wa vyandarua bure ni mkakati muhimu katika kupunguza maambukizi ya malaria na kulinda afya za wananchi, hasa makundi yaliyo hatarini kama watoto na wajawazito.

Aidha, amewataka watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha kuwa vyandarua vinawafikia walengwa wote kwa wakati na vinatumika ipasavyo kwa lengo lililokusudiwa, ameonya dhidi ya matumizi mabaya ya vyandarua, akisisitiza kuwa vinapaswa kutumika kulinda afya na si kwa shughuli nyingine zisizohusiana.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kampeni ya Ugawaji Vyandarua Ngazi ya Kaya bila Malipo kutoka Wizara ya Afya, Bw. Wilfred Mwafongo, amewahimiza viongozi wa dini kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi ya vyandarua katika kuzuia malaria, amesema ushiriki wa viongozi hao ni muhimu kwa kuwa wana nafasi kubwa ya kuifikia jamii kwa urahisi.

Hatahivyo Bw. Mwafongo ameongeza kuwa jumla ya vyandarua 224,339 vinatarajiwa kusambazwa kwa kaya 112,556 ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambapo zoezi hilo ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kutokomeza malaria na litasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi na madhara yatokanayo na ugonjwa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SERIKALI YAIMARISHA USAMBAZAJI WA CHANJO IKIZINDUA BOTI 7 ZA BILION1.1

Serikali imeendelea kuimarisha huduma za chanjo nchini kupitia uzinduzi wa boti saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.1...

VYOMBO VYA HABARI NCHINI VYA TAJWA KUWA NGUZO YA KULINDA MAADILI YA MTANZANIA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali inavitegemea kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari...

UZALISHAJI NA UINGIZAJI WA MIFUKO YA PLASTIKI WAPUNGUA KWA ASILIMIA 95%

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Reuben Kwagilwa bungeni jijini...

WANAFUNZI KATAVI WATAKIWA KUONYESHA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kishaki iliyopo Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la...