Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kishaki iliyopo Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za matukio mbalimbali ya kihalifu yakiwemo ya ukatili na unyanyasaji wa Kijinsia.
Wito huo umetolewa Aprili 29, 2026 na Mtendaji wa Dawati la Jinsia na watoto la Wilaya ya Mpanda, Sajenti Yunis Magelo Wakati akitoa elimu ya namna ya kuzuia ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi na kuwataka waepuke kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo.
Hatahivyo Sajenti Yunis amewataka wanafunzi hao kuwa na maadili mema katika jamii zinazowazunguka ikiwemo kuepuka kujihusisha na makundi ya kihalifu badala wasome kwa bidii ili kutimiza malengo yao ya baadae.






