Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesema huduma ya intaneti ya kasi imefikia asilimia 94 ya maeneo ya makazi nchini, huku idadi ya watumiaji wa intaneti ikiongezeka na kufikia asilimia 85.3.
Akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 30, 2026, Waziri Kairuki amesema Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya mawasiliano kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
Ameeleza kuwa uwezo wa Mkongo wa Taifa umeongezwa kutoka 200Gbps hadi kati ya 400Gbps na 2,000Gbps kwenye njia kuu, huku maunganisho ya mipakani yakiongezwa kutoka 100Gbps hadi 800Gbps ili kuongeza kasi, ufanisi na upatikanaji wa huduma za mtandao nchini.






