MeTL YATOA KAULI UTEKELEZAJI AGIZO LA SERIKALI

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA – 0711 46 49 84

KAMPUNI ya Mohamed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) inayomiliki mashamba ya mkonge yaliyoko Tanga, imesema inatekeleza kwa awamu agizo la Serikali la kuyaendeleza mashamba hayo.

Mmoja wa maofisa wa kampuni hiyo ameeleza kuwa baada ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula kuipa siku 24 za kuyaendeleza mashamba hayo ilianza kuliyafanyia kazi agizo hilo.

Afisa huyo alisema uendelezaji huo unafanyika kwa awamu kwa sababu siyo jambo rahisi kuliendeleza eneo lote kwa wakati mmoja na tayari imekwishawasilisha mpango wake ya kuyaendeleza mashamba hayo kwa Serikali.

Maelezo hayo yanajibu taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Sekta ya Katani kuwa agizo la Serikali lililotolewa na Naibu Waziri Mabula, halijatekelezwa tangu mwaka jana ingawa kampuni hiyo iliandika barua serikalini ikieleza namna itakavyotekeleza kwa awamu uendelezaji huo.

Disemba 8, mwaka jana, MeTL ilipewa siku 24 na Serikali kuyaendeleza mashamba hayo yenye ukubwa wa hekta 9,418 ambayo miongoni mwake hayajaendelezwa na badala yake yamegeuka kuwa pori.

Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Stephen Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Majimarefu ambaye aliambatana na Naibu Waziri Mabula katika ziara hiyo ya mwaka jana, alieleza kuwa MeTL ilimilikishwa mashamba hayo mwaka 2000 lakini tangu wakati huo ilishindwa kuyaendeleza kikamilifu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...