LONDON, Uingereza
MIKEL Arteta ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza katika historia ya Arsenal kuiwezesha timu hiyo kutinga mara mbili mfululizo hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Arsenal walivuka robo fainali usiku wa jana Aprili 15, 2026 baada ya kulazimishwa suluhu na Sporting Lisbon pale Emirates.

Washika Bundiki wameingia nusu fainali kwa matokeo ya robo fainali ya kwanza, walipoifunga Lisbon bao 1-0 kule Ureno.

Arteta aliiongoza Arsenal kufika nusu fainali msimu uliopita (2024-25) lakini safari yao ya kwenda fainali ilikwamishwa na PSG.

Kwa upande mwingine, hii inakuwa mara ya pili tangu msimu wa 2008-09 kwa Arsenal kufika nusu fainali ya mashindano hayo.

Mara ya mwisho kwao kukanyaga hatua hiyo walifungwa jumla ya mabao 4-1 katika mechi mbili (nyumbani na ugenini) walizocheza dhidi ya Manchester United.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here