Thursday, 8 October 2026

MAKABIDHIANO YA UWONGOZI TWPG YAFANYIKA RASMI

Makabidhiano ya uongozi wa Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) kwa kipindi kipya cha mwaka 2026 hadi 2030 yamefanyika rasmi, yakihitimisha uongozi wa miaka mitano uliodumu kuanzia 2021 hadi 2025 na kufungua awamu mpya ya uongozi. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Bunge, ambapo Katibu Mkuu mstaafu, Mhe. Agnes Hokororo, amekabidhi rasmi majukumu kwa Katibu Mkuu […]

Makabidhiano ya uongozi wa Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) kwa kipindi kipya cha mwaka 2026 hadi 2030 yamefanyika rasmi, yakihitimisha uongozi wa miaka mitano uliodumu kuanzia 2021 hadi 2025 na kufungua awamu mpya ya uongozi.

Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Bunge, ambapo Katibu Mkuu mstaafu, Mhe. Agnes Hokororo, amekabidhi rasmi majukumu kwa Katibu Mkuu mpya, Mhe. Dkt. Catherine Joachim, anayechukua nafasi hiyo kwa kipindi kipya.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Kamati ya Utendaji ya TWPG chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa umoja huo, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako. Aidha, Naibu Katibu Mkuu mstaafu, Mhe. Cecilia Pareso, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Kumi na Tatu, alihudhuria tukio hilo.

Tukio hilo linaashiria mwendelezo wa uongozi thabiti, uwajibikaji wa taasisi pamoja na dhamira ya kuimarisha utendaji wa TWPG katika kipindi hiki kipya cha Bunge la 13.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *