LONDON, Uingereza
ZIPO taarifa kuwa kocha wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard, aanawindwa na mabosi wa klabu ya Bournemouth ya Ligi Kuu ya England (EPL).
Bournemouth wanasaka kocha wa kuliongoza benchi la ufundi baada ya Andoni Iraola kusema ataachia ngazi mwishoni mwa msimu huu.
Lampard amekuwa na mafanikio makubwa tangu alipoanza kuinoa Coventry City, akiifanya timu hiyo kuwa tishio Ligi Daraja la Kwanza England (Championship).
Timu yake hiyo iko kileleni mwa msimamo wa Championship kwa tofauti ya pointi 10, zikiwepo dalili zote za kutwaa ubingwa wao wa kwanza baada ya miaka 25 kupita.
Makocha wengine wanaotajwa kuingia kwenye rada za klabu hiyo ni Kieran McKenna, Marco Rose na Inigo Martinez.






