MERSEYSIDE, Uingereza
KICHAPO cha mabao 2-0 kutoka kwa PSG kimeongeza presha kwa kocha wa Liverpool, Arne Slot, ikielezwa kuwa huenda Mholanzi huyo akafungashiwa virago hivi karibuni.
Wakiwa nyumbani Anfield, Liverpool walikubali kipigo hicho kilichowasukuma nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, waliishia hatua ya robo fainali.
Katika mechi ya kwanza iliyocheza jijini Paris wiki moja iliyopita, PSG walipata ushindi kama huo, hivyo sasa wametinga hatua ya nusu fainali.
Kwa matokeo hayo, Liverpool imefikisha mechi 17 ilizopoteza msimu huu, takwimu zinazoongeza presha kwa Slot kutimuliwa.
Kocha anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba yake pale Anfield ni kiungo wa zamani wa klabu za Liverpool, Bayern Munich na Real Madrid, Xabi Alonso.






