BEKI NEWCASTLE ASAKWA NA VIGOGO ULAYA

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza

SAINI ya beki wa kushoto wa Newcastle United, Lewis Hall, inawindwa na klabu kadhaa kubwa za Ulaya, zikiwemo za Ligi Kuu ya England (La Liga).

Kwa mujibu wa ripoti, klabu zinazopigana vikumbo kuisaka huduma yake ni Chelsea, Arsenal, Manchester City, Manchester United, Liverpool, Barcelona, na Real Madrid.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, ameshacheza mechi 42 akiwa na kikosi hicho cha kocha Eddie Howe tangu kuanza kwa msimu huu.

Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Newcastle hawana mpango wa kumuuza na badala yake wanahaha kumshawishi aongeze mkataba.

Mkataba wake na Newcastle unaisha mwaka 2029 na endapo klabu hiyo italazimika kumuuza, basi itahitaji si chini ya Pauni milioni 55.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...