LONDON, Uingereza
MECHI mbili za marudiano za hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zitachezwa usiku wa leo, kabla ya zingine (2) kuchezwa kesho.
Leo Aprili 14, Atletico Madrid na Barcelona zitarudiana baada ya Wacatalunya kushinda mabao 2-0 wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Camp Nou. Je, Barca ‘watapindua meza’ wakiwa ugenini?
Mchezo mwingine wa leo ni ule Liverpool dhidi ya PSG utakaochezwa Anfield. Mechi ya kwanza ilichezwa Anfield na PSG kushinda mabao 2-0.
Kesho Aprili 15, 2026, Bayern watakuwa nyumbani kuivaa Real Madrid. Bayern walishinda mabao 2-1 katika mechi ya kwanza wakiwa ugenini Santiago Bernabeu.
Pia, Arsenal watakuwa Emirates kuvaana na Sporting Lisbon baada ya Washika Bunduki hao kushinda bao 1-0 kule Ureno.
Imeandaliwa na Hassan Mwasha






