Wednesday, 7 October 2026

JE MIKEL ARTETA AMEKALIA KUTI KAVU ARSENAL?

LONDON, UingerezaIMEFICHUKA kuwa mabosi wa Arsenal wameanza kusaka mrithi wa kocha wa sasa, Mikel Arteta. Ripoti zinaeleza kuwa mabosi wa Arsenal hawatovumilia endapo timu yao itaambulia patupu msimu huu. Arsenal iko kwenye mbio za kuwania mataji makubwa mawili; Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa. Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa, tayari timu hiyo iko robo […]

LONDON, Uingereza
IMEFICHUKA kuwa mabosi wa Arsenal wameanza kusaka mrithi wa kocha wa sasa, Mikel Arteta.

Ripoti zinaeleza kuwa mabosi wa Arsenal hawatovumilia endapo timu yao itaambulia patupu msimu huu.

Arsenal iko kwenye mbio za kuwania mataji makubwa mawili; Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa.

Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa, tayari timu hiyo iko robo fainali, wakati inaongoza kwa pointi sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Ikumbukwe, Arsenal walikuwa na nafasi nzuri ya kutwaa Kombe la Ligi (EFL Cup) lakini walifungwa mabao 2–0 na Southampton katika mchezo wa fainali.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *