Friday, 21 August 2026

CHERKI WA MAN CITY AWEKA REKODI

MANCHESTER, Uingereza ‘ASISTI’ zake katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Chelsea zimemfanya kiungo wa Manchester City, Rayan Cherki, kuweka rekodi mpya Ligi Kuu England (EPL). Man City ikiwa ugenini Stamford Bridge, ilipata ushindi huo, hivyo kubakiza pointi sita kuifikia Arsenal iliyoko kileleni mwa msimamo. Cherki ndiye aliyepiga asisti katika mabao mawili, wafungaji wakiwa ni […]

MANCHESTER, Uingereza

‘ASISTI’ zake katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Chelsea zimemfanya kiungo wa Manchester City, Rayan Cherki, kuweka rekodi mpya Ligi Kuu England (EPL).

Man City ikiwa ugenini Stamford Bridge, ilipata ushindi huo, hivyo kubakiza pointi sita kuifikia Arsenal iliyoko kileleni mwa msimamo.

Cherki ndiye aliyepiga asisti katika mabao mawili, wafungaji wakiwa ni Nico O’Reilly na Marc Guehi. Bao jingine lilipachikwa na Jeremy Doku.

Anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya EPL kufikisha asisti 10 katika msimu wake wa kwanza EPL tangu Dimitri Payet alipofanya hivyo msimu wa 2015-16.

Kiungo mshambuliaji huyo alijiunga na Man City mwaka jana akitokea Lyon ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *