HII HAPA ORODHA YA MAKOCHA WA SOKA MATAJIRI ZAIDI DUNIANI

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza

SOKA ndiyo mchezo unaopendwa na kufutatiliwa zaidi duniani, hiyo ikisababisha wachezaji na makocha kuishi kifahari kutokana na fedha nyingi wanazovuna.

Katika makala haya, hawa ni makocha wanaotajwa kuwa matajiri zaidi duniani. Ni akina nani hao?

DIEGO SIMEONE

Ndiye kocha mwenye mkwanja mrefu zaidi duniani, akiwa na utajiri wa Pauni milioni 102. Simeone amekuwa kocha wa Atletico Madrid tangu mwaka 2011.

Mkataba wake wa sasa utafikia ukomo mwaka 2027 na zipo ripoti zinazodai kuwa ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

JOSE MOURINHO

‘Special One’ ana utajiri wa Pauni milioni 100. Sehemu kubwa ya utajiri wake umetokana na fidia alizolipwa katika klabu alizowahi kufukuzwa.

Mathalan, Mourinho aliweka mfukoni kitita cha Pauni milioni 17 alipovunjiwa mkataba na Chelsea mwaka 2017.

PEP GUARDIOLA

Kama ilivyo kwa Mourinho, Guardiola wa Manchester City naye ana utajiri wa Pauni milioni 100.

Ripoti zinaeleza kuwa huenda akaondoka Etihad mwishoni mwa msimu huu, ingawa Mhispania huyo hajasema chochote juu ya hatima yake.

ZINEDINE ZIDANE

Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid ana utajiri wa Pauni milioni 91.6, licha ya kwamba amekuwa nje ya kazi tangu alipoondoka klabuni hapo mwaka 2021.

‘Zizou’ anahusishwa na kibarua cha kuinoa timu ya Taifa ya Ufaransa baada ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.

CARLO ANCELOTTI

Utajiri wake ni Pauni milioni 41 na kwa sasa Muitalia huyo anainoa timu ya Taifa ya Brazil ‘Selecao’ (Wateule).

Ancelotti alianza kazi ya ukocha mwaka 1995. Ana umri wa miaka 66 baada ya miaka 31 ya kufanya kazi hiyo.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...