Monday, December 23, 2024
spot_img

SERIKALI KUHUISHA ANWANI ZA MAKAZI MILIONI 12.3

RIPOTA WA WHMTH

Arusha

SERIKALI  imekusanya taarifa za Anwani za Makazi Milioni 12.3 zinazotakiwa kuhuishwa kila wakati ili ziendelee kuwa taarifa sahihi wakati wote kwa kuwa zinabadilika mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nicholaus Merinyo Mkapa, 14 Agosti, 2024 wakati wa ufunguzi wa uhakiki wa taarifa za Anwani za Makazi mkoani Arusha.

Mkapa amesema ni lazima iwepo mikakati endelevu ya kuhakikisha mfumo wa Anwani za Makazi (NaPA) unakuwa na taarifa sahihi kila wakati kwa kuwa nyumba mpya zinajengwa kila siku, upimaji wa viwanja unaendelea katika maeneo mbalimbali, watu wanahama kutoka eneo moja kwenda jingine, matumizi yanabadilika na sababu nyingine kadhaa.

“Katika kufanikisha suala hilo, wizara imeandaa mkakati wa kufanya uhakiki wa taarifa katika halmashauri zote nchini (mass data cleaning), unaokwenda sambamba na kujenga uwezo kwa waratibu, wataalamu wenyeviti na watendaji wa kata na mitaa ili waweze kuendelea kutekeleza shughuli za mfumo wa Anwani za Makazi katika maeneo yao”, amesema Mkapa.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema hadi sasa wizara imeshafanya uhakiki na kujenga uwezo katika halmashauri 31, kati ya hizo 19 ni za Tanzania Bara na 11 za Zanzibar.            

Amesema katika uhakiki huo, wizara imefanikiwa kuhuisha zaidi ya taarifa za anwani milioni 2.3, kutoa anwani mpya zaidi ya 500,000 na kujenga uwezo kwa wataalamu, wenyeviti na watendaji 6,621.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano wa Wizara hiyo, Mulembwa Munaku amesema kuwa uhakiki unafanyika baada ya wizara kufanya tathmini na kubainisha mapungufu mbalimbali yakiwemo baadhi ya taarifa zilizokusanywa kukosa sifa, kutoa majina ya barabara bila kuzingatia miongozo na baadhi ya wananchi kutofikiwa na zoezi.

Munaku amesema ufunguzi uliofanyika leo unakwenda sambamba na utoaji wa mafunzo kwa washiriki ambapo mada mbalimbali zitatolewa kama vile utambuzi na utoaji wa majina ya barabara na namba za anwani, mfumo wa kidijitali wa Anwani za Makazi, kupata uelewa wa maswali yanayotumika kukusanya taarifa za anwani na utaratibu wa kusajili na kuhakiki majina wa barabara

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya