Thursday, 20 August 2026

RAIS SAMIA KUZINDUA MRADI WA JNHPP AGOSTI 22

RIPOTA PANORAMA RAIS Samia Suluhu Hassana anatarajiwa kuzindua bwawa la kuzalisha umeme wa megawati 2,115 lililopo Rufuji, Mkoa wa Pwani, Agosti 22, 2026. Akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo za Wizara ya Nishati, Agosti…

RIPOTA PANORAMA

RAIS Samia Suluhu Hassana anatarajiwa kuzindua bwawa la kuzalisha umeme wa megawati 2,115 lililopo Rufuji, Mkoa wa Pwani, Agosti 22, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo za Wizara ya Nishati, Agosti 15, 2026 Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi alisema uzindyuzi wa bwawa hilo linalofahamika kwa jina la Juluius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) utakaohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
serikali, wageni kutoka nje ya nchi, wananchi na wadau wa maendeleo.

“Uzinduzi huu wa mradi wa umeme wa  Julius Nyerere ni tukio la kihistoria na hatua muhimu katika safari ya Tanzania ya kujenga mfumo wa nishati ya uhakika nchini, sambamba na kuchochea shughuli za uzalishaji, uwekezaji na ukuaji wa uchumi.

“Huu ni mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme kuwahi kutekelezwa nchini kwa kutumia fedha za ndani za Serikali ukiwa na uwekezaji wa takribani Shilingi trilioni 7.452,” alisema Ndejembi

Alisema JNHPP imeongeza kiwango cha umeme kinachoingia katika Gridi ya Taifa hivyo kupunguza changamoto za upungufu wa uzalishaji zilizokuwa zikichangia mgao wa umeme nchini.

Waziri Ndejembi alisema hadi Mei 31, 2026, JNHPP ilikuwa imezalisha takribani asilimia 44.9 ya umeme wote uliozalishwa na kuingia katika Gridi ya Taifa kwa kipindi cha mwaka mmoja. Kwamba hilo linaonyesha kuwa nusu ya umeme unaotumika nchini unatoka kwenye bwawa hilo.

Kuhusu gharama za mradi, Waziri Ndejembi alisema fedha iliyotumika ni takriban Dola za Marekani Bilioni 3.35 sawa na Shilingi za Tanzania trilioni 7.452.

Alisema pamoja na mradi huo mahususi kwa ajili ya kufua umeme, utasaidia pia kwenye kudhibiti mafuriko katika mto Rufiji, kilimo cha umwagiliaji, utalii na matumizi ya
binadamu.

Ujenzi wa mradi wa JNHPP ulianza Juni, 2019 na kukamilika Machi, 2025. Uwezo wa bwawa la kutunza maji ni mita za ujazo bilioni 33 (mara 10 zaidi ya uwezo wa bwawa la Mtera).

Bwawa hilo ni ziwa la kujenga na linashika nafasi ya nne kwa ukubwa katika maziwa yaliyoko nchini, baada ya Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa huku kituo cha kuzalisha umeme cha JNHPP kikishika nafasi ya nne kwa ukubwa katika Bara la Afrika.


About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *