RIPOTA PANORAMA
Zanzibar
WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema usambazaji teknolojia ya nishati safi ya kupikia, unapaswa kwenda sambamba na mabadiliko ya mila, desturi na mitazamo inayochangia kuzorotesha juhudi za serikali za kuwawezesha wananchi wote kutumia nishati safi ya kupikia.
Akizungumza Agosti 11, 2026 kwenye mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF), na kuwakutanisha wadau kutoka sekta binafsi, washirika wa maendeleo, taasisi za fedha, serikali, wanateknolojia, watafiti na asasi za kiraia, huko Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibari, waziri huyo alisema ni muhimu kubadili mitizamo kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.
“Licha ya kuwa na mkakati wa nishati safi ya kupikia, tusipowekeza katika kubadili mila na desturi zetu tutajikuta pale pale. Wakati tunasukuma matumizi ya teknolojia, tuwekeze pia katika kubadili mitazamo ya watanzania kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia,” alisema Ndejembi.

Alisisitiza kuwa mabadiliko yanahitaji ushirikiano wa serikali, taasisi na jamii yenyewe ili kuondoa mitazamo na desturi zinazoweza kuwa kikwazo katika kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Aidha, aliwaasa watendaji wa wizara, taasisi na sekta binafsi kuweka kipaumbele kwenye matumizi ya teknolojia mchanganyiko za nishati safi ya kupikia kulingana na rasilimali zinazopatikana katika maeneo husika na kutoa mfano wa maeneo yenye samadi ambayo inaweza kutumika kuzalisha bayogesi ili kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia.
wakati wa mdahalo wa nishati safi ulioandaliwa na ulikutanisha na ulilenga kujadili namna ya kuongeza kasi ya upatikanaji na matumizi ya nishati safi ya kupikia iliyo endelevu na nafuu kwa wananchi na taasisi.
Kwa mujibu wa Waziri Ndejembi, hivi sasa watanzania wanaotumia nishati safi ya kupikia ni asilimia 28.6 kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021.
Mwisho.

