KLABU ya Simba imemtambulisha rasmi winga kijanaM, Bakari Msimu kama mchezaji mpya wa timu hiyo baada ya kukamilisha usajili akitokea Klabu ya Coastal Union.
Msimu amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomuweka ndani ya Simba hadi mwaka 2028.
Usajili wa winga huyo ni sehemu ya mkakati wa Simba kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) pamoja na mashindano ya kimataifa.
Msimu anaonekana kuwa miongoni mwa vipaji vinavyochipukia kwa kasi katika soka la Tanzania, jambo ambalo limeongeza matarajio makubwa kwa mashabiki wa Simba wanaosubiri kuona mchango wake ndani ya kikosi hicho.
Kupitia usajili huo, Simba SC inalenga kuongeza ushindani na ubora katika safu yake ya ushambuliaji huku ikiendelea kujenga kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao

