Thursday, 20 August 2026

FUJO ZAZUKA LONDON BAADA YA MOROCCO KUAGA KOMBE LA DUNIA

Vurugu zimeripotiwa kuzuka katika eneo la Edgware Road, jijini London, Uingereza, baada ya mashabiki wa Morocco kuonesha hasira kufuatia timu yao kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2026 na Ufaransa. Kwa mujibu wa taarifa…

Vurugu zimeripotiwa kuzuka katika eneo la Edgware Road, jijini London, Uingereza, baada ya mashabiki wa Morocco kuonesha hasira kufuatia timu yao kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2026 na Ufaransa.

Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, mamia ya mashabiki walikusanyika katika eneo hilo kutazama mchezo huo, lakini hali ilibadilika na kuwa ya taharuki baada ya Morocco kupoteza.

Video zilizosambaa mtandaoni zinaonesha baadhi ya watu wakikimbia barabarani, huku wengine wakidaiwa kurusha vitu na kukabiliana na polisi waliokuwa wakijaribu kurejesha utulivu.

Taarifa hizo pia zinadai kuwa askari mmoja alianguka wakati wa tukio hilo, huku baadhi ya maafisa wa usalama wakilazimika kujiondoa kwa muda kutokana na msongamano wa watu.

Hata hivyo, hadi sasa mamlaka za Uingereza hazijatoa taarifa rasmi kuhusu idadi ya waliokamatwa, waliojeruhiwa au kiwango cha uharibifu uliotokea.

Polisi wanaendelea na uchunguzi huku wakitoa wito wa kudumishwa kwa amani.

Morocco iliaga Kombe la Dunia 2026 baada ya kufungwa na Ufaransa, matokeo yaliyowaacha mashabiki wake wengi wakiwa na huzuni, huku baadhi yao wakihusishwa na vurugu zilizotokea London.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *