Thursday, 20 August 2026

UTAPENDA ALICHOKIFANYA MBAPE KWA WACHEZAJI WA MOROCCO

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappé, akiwapa moyo wachezaji wa Morocco baada ya mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia imezua hisia kwa mashabiki wengi duniani. Baada ya…

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappé, akiwapa moyo wachezaji wa Morocco baada ya mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia imezua hisia kwa mashabiki wengi duniani.

Baada ya mchezo huo ambao Ufaransa iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Morocco, Mbappé alionekana akizungumza maneno ya faraja na kuwapa pole wachezaji kadhaa wa timu hiyo, akiwemo Achraf Hakimi, Brahim Díaz na Yassine Bounou.

Tukio hilo limeelezwa na wengi kama mfano wa heshima na uungwana katika soka, likionesha ukomavu wa wachezaji hao pamoja na uhusiano mzuri uliopo baina yao nje ya uwanja licha ya ushindani wa ndani ya mchezo.

Kitendo cha Mbappé kimeendelea kusifiwa na mashabiki wengi, wakikitaja kama ujumbe wa mshikamano, heshima na thamani halisi ya mchezo wa soka.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *