Tuesday, 25 August 2026

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA SITA AFRIKA MASHARIKI HAKI ZA KIDIJITALI

Tanzania imeshika nafasi ya sita miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki katika viwango vya kulinda haki za kidijitali na kukuza ujumuishi wa kidijitali, kwa mujibu wa ripoti ya Londa: Digital Rights and Inclusion in Africa Report 2024. Taarifa hiyo ilitolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Programu wa Paradigm Initiative Afrika Mashariki wakati wa […]

Tanzania imeshika nafasi ya sita miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki katika viwango vya kulinda haki za kidijitali na kukuza ujumuishi wa kidijitali, kwa mujibu wa ripoti ya Londa: Digital Rights and Inclusion in Africa Report 2024.

Taarifa hiyo ilitolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Programu wa Paradigm Initiative Afrika Mashariki wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu haki za kidijitali.

Amesema tathmini hiyo ilibaini kuwa nchi za Afrika Mashariki zimeonesha viwango tofauti katika kulinda haki za kidijitali na kuhakikisha wananchi wanapata fursa sawa za kutumia teknolojia za kidijitali.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania ilipata alama 20 kati ya 60, ikiwa ni alama za chini zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Ameeleza kuwa pamoja na kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za intaneti, bado kuna changamoto zinazohusisha uhuru wa kujieleza mtandaoni, haki ya faragha na upatikanaji wa taarifa.

Ameeleza umuhimu wa wadau mbalimbali kushirikiana katika kuimarisha mifumo ya kulinda haki za kidijitali ili kuhakikisha maendeleo ya teknolojia yanakwenda sambamba na ulinzi wa haki za wananchi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *