Monday, 24 August 2026

RAIS WA SENEGAL AZIPONGEZA TIMU ZA U17 NA U15 BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA AFRICA

‎Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amezipokea timu za taifa za vijana za U17 na U15 kufuatia mafanikio yao ya kutwaa ubingwa wa Afrika katika mashindano ya vijana.‎‎Katika hafla maalumu iliyofanyika muda mchache uliopita , Rais Faye aliwapongeza wachezaji, na benchi la ufundi kwa kuiletea Senegal heshima kubwa kupitia mafanikio yao ya kipekee.‎‎‎ Aidha Serikali […]

‎Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amezipokea timu za taifa za vijana za U17 na U15 kufuatia mafanikio yao ya kutwaa ubingwa wa Afrika katika mashindano ya vijana.

‎Katika hafla maalumu iliyofanyika muda mchache uliopita , Rais Faye aliwapongeza wachezaji, na benchi la ufundi kwa kuiletea Senegal heshima kubwa kupitia mafanikio yao ya kipekee.


‎ Aidha Serikali ya Senegal pia ilitoa zawadi za fedha ambapo timu ya U17 ilipokea kiasi cha faranga za CFA milioni 179.5, huku timu ya U15 ikikabidhiwa faranga za CFA milioni 131.9.

‎Hatua hiyo inaonesha dhamira ya serikali ya Senegal katika kuendeleza na kuthamini vipaji vya vijana vinavyoitangaza nchi kimataifa kupitia michezo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *