‎Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Hussein Mohammed, ameungana na wachezaji, makocha, waamuzi wa mechi pamoja na wadau mbalimbali wa soka katika hafla ya utoaji wa Tuzo za SportPesa League 2025/26 zilizofanyika kenya kwa lengo la kutambua na kusherehekea waliofanya vizuri zaidi katika msimu uliomalizika.

‎Katika hafla hiyo, washindi na walioteuliwa katika tuzo mbalimbali walipongezwa kwa juhudi, kujituma na mchango wao mkubwa katika kuimarisha kiwango cha soka nchini Kenya.

‎Kwa upande wa  FKF imeeleza kuwa mafanikio ya washiriki hao yanaendelea kuinua hadhi ya ligi na kuchochea maendeleo ya mchezo huo.

‎Shirikisho hilo pia limesisitiza dhamira yake ya kuendelea kukuza soka la Kenya kwa kuimarisha ushindani wa ligi na kuweka mazingira bora yatakayoiwezesha ligi hiyo kuwa miongoni mwa ligi bora zaidi barani Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here