‎Klabu ya Beşiktaş ya Uturuki imefikia makubaliano na kocha raia wa Italia, Vincenzo Italiano, kumteua kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu utakaodumu hadi Juni 2028.

‎Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na mwanahabari maarufu wa masuala ya usajili, Fabrizio Romano, Italiano anatarajiwa kuwasili Istanbul leo ili kusaini mkataba wake rasmi na kuanza majukumu mapya ndani ya klabu hiyo.

‎Kocha huyo, ambaye amekuwa akifanya vizuri katika soka la Italia akiwa na Bologna, atalipwa mshahara wa euro milioni 6 kwa msimu.

‎Aidha, tayari amekubaliana na uongozi wa Beşiktaş kuhusu benchi lake la ufundi, jambo linaloashiria maandalizi ya haraka kuelekea msimu mpya wa mashindano.

‎Ujio wa Vincenzo Italiano unatajwa kuwa sehemu ya mkakati wa Beşiktaş wa kuimarisha kikosi chake na kurejesha ushindani katika ligi kuu ya Uturuki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here