‎Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amesema kuwa mpira wa miguu una uwezo mkubwa wa kuunganisha watu na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

‎ Kupitia ushirikiano kati ya FIFA, Bank of America na Vet Tix, wanajeshi wastaafu pamoja na familia zao watapata nafasi ya kushuhudia na kushiriki katika mazingira ya mashindano ya FIFA World Cup 2026.

‎Mpango huo unakuja wakati United States ikijiandaa kuadhimisha miaka 250 ya taifa hilo sambamba na maandalizi ya Kombe la Dunia la 2026.

‎Aidha FIFA imesisitiza kuwa lengo la ushirikiano huo ni kuwapa heshima na shukrani wanajeshi na familia zao kwa mchango wao kwa taifa, huku ikihakikisha wanapata fursa ya kuwa sehemu ya tukio kubwa zaidi la soka duniani.

‎Kwa mujibu wa FIFA, mpira wa miguu si mchezo pekee bali ni chombo cha kuleta umoja, matumaini na maendeleo katika jamii mbalimbali duniani kote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here