Klabu ya Liverpool F.C. inatarajiwa kumtangaza rasmi Andoni Iraola kuwa kocha wake mpya baada ya kufikia makubaliano ya mkataba wa miaka miwili utakaodumu hadi Juni 2028.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na mwanahabari maarufu wa masuala ya usajili Fabrizio Romano, makubaliano kati ya Liverpool na kocha huyo wa Hispania yamekamilika, huku utambulisho wake rasmi ukitarajiwa kufanyika ndani ya wiki hii.
Aidha Iraola anatarajiwa kuchukua nafasi ya Arne Slot, ambaye ameiongoza Liverpool katika kipindi cha hivi karibuni.
Pia kocha huyo ameonyesha nia ya kuambatana na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu katika benchi la ufundi, akiwemo Pablo de la Torre, Tommy Elphick, Shaun Cooper na Tom Webber.







