‎Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa Atalanta, Ederson, katika dirisha la usajili la majira ya joto.

‎Kwa mujibu wa taarifa hizo, United italipa euro milioni 45 pamoja na nyongeza mbalimbali ili kukamilisha uhamisho wa nyota huyo wa Brazil.

‎ Aidha Ederson anatajwa kuwa niusajili wa kwanza chini ya kocha Michael Carrick katika maandalizi ya msimu mpya.

‎Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yalidumu kwa wiki kadhaa kabla ya kufikia hatua ya makubaliano ya mwisho.

‎ Mchezaji huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne mara baada ya kukamilisha vipimo vya afya na taratibu nyingine za mwisho za uhamisho.

‎Usajili wa Ederson ni sehemu ya mkakati wa Manchester United wa kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao, huku mashabiki wakisubiri kuona mchango wake ndani ya dimba la Old Trafford.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here