Klabu ya Bayern Munich imepiga hatua kubwa katika harakati za kumsajili kiungo mshambuliaji wa PSV Eindhoven, Ismael Saibari, baada ya kufikia makubaliano ya awali kuhusu masuala binafsi ya mchezaji huyo.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari tofauti tofauti vya eleza usajili wa mchezaji, Fabrizio Romano, Saibari amekubali kujiunga na Bayern kwa mkataba wa miaka mitano baada ya mazungumzo yaliyofanyika moja kwa moja na kocha wa klabu hiyo, Vincent Kompany.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa mchezaji huyo raia wa Morocco ameonesha nia ya kuhamia Bayern Munich, huku suala la mshahara likiwa tayari limekubaliwa kati ya pande husika.
Hata hivyo, makubaliano ya mwisho bado hayajakamilika kwani Bayern Munich na PSV Eindhoven zinaendelea na mazungumzo kuhusu ada ya usajili wa mchezaji huyo.
Iwapo mazungumzo hayo yatakamilika kwa mafanikio, Saibari anatarajiwa kuwa mmoja wa nyota wapya watakaojiunga na Bayern Munich kuelekea msimu ujao.







