‎Klabu ya Real Madrid imefikia hatua ya mwisho katika harakati za kumsajili beki wa kulia Denzel Dumfries kutoka Inter Milan, kulingana na taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

‎‎Taarifa hiyo inaeleza kuwa Real Madrid tayari wamekubaliana masharti binafsi na Dumfries, hatua inayomweka mchezaji huyo karibu zaidi na kuhamia katika klabu hiyo ya Hispania.

‎Aidha baada ya kukamilisha makubaliano hayo, Madrid inadaiwa kuwa tayari kulipa euro milioni 20 ambazo zinatajwa kuwa ni kipengele cha kuachiliwa kwa mchezaji huyo.

‎Dumfries, ambaye ni nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Netherlands, amekuwa mmoja wa mabeki wa kulia wanaofanya vizuri barani Ulaya kutokana na uwezo wake wa kushambulia na kusaidia safu ya ulinzi ya timu yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here