‎Mchezaji mkongwe wa soka nchini England, James Milner, ametangaza rasmi kustaafu soka la kulipwa baada ya kuwa na mafanikio makubwa ndani ya Ligi Kuu ya England.

‎Milner anaondoka akiwa ndiye mchezaji aliyeshiriki mechi nyingi zaidi katika historia ya Premier League, akicheza jumla ya mechi 658 katika kipindi chake chote cha soka la kulipwa.

‎Aidha kiungo huyo aliyewahi kuzitumikia klabu mbalimbali za England alijijengea heshima kutokana na kiwango chake bora, nidhamu na uwezo wake wa kudumu katika kiwango cha juu kwa miaka mingi.

‎Tangazo la kustaafu kwake limepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa soka duniani, wengi wakimpongeza kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya mchezo huo na mafanikio aliyoyapata katika maisha yake ya soka.

‎Milner anaondoka akiwa mmoja wa wachezaji walioweka alama ya kudumu katika historia ya Premier League kutokana na rekodi na mchango wake mkubwa ndani ya mchezo wa soka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here