Wednesday, 26 August 2026

WANAFUNZI 7 WATAMBULIWA KAMA WASHUKIWA WA MOTO KATIKA BWENI LA WANAFUNZI KENYA

Polisi nchini Kenya imetangaza kuwatambua rasmi wanafunzi saba kama washukiwa wakuu wa tukio la uchomaji moto bweni la wasichana katika shule ya bweni lililotokea wiki iliyopita na kusababisha vifo vya wanafunzi 16. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumapili, Mei 31, uchunguzi wa awali umebaini kuwa wanafunzi hao walihusika na tukio hilo baada ya picha za […]

Polisi nchini Kenya imetangaza kuwatambua rasmi wanafunzi saba kama washukiwa wakuu wa tukio la uchomaji moto bweni la wasichana katika shule ya bweni lililotokea wiki iliyopita na kusababisha vifo vya wanafunzi 16.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumapili, Mei 31, uchunguzi wa awali umebaini kuwa wanafunzi hao walihusika na tukio hilo baada ya picha za kamera za usalama kuwaonesha katika mazingira yanayohusishwa na moto huo. Polisi hawajataja majina ya washukiwa hao kutokana na sababu za kisheria.

Katika mkasa huo uliotokea Jumatano iliyopita, wanafunzi 16 walipoteza maisha huku wengine kadhaa wakijeruhiwa, Moto huo ulizuka katika ghorofa ya kwanza ya bweni la wasichana ambalo lilikuwa na jumla ya vitanda 135.

Polisi wamesema washukiwa sita walikuwa tayari wamekamatwa kufikia jana, huku mshukiwa wa saba akikabidhiwa kwa mamlaka na wazazi wake kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi.

Aidha, uchunguzi wa miili ya marehemu wote umekamilika na umebaini kuwa vifo hivyo vilitokana na majeraha makubwa ya kuungua baada ya miili yao kuteketea vibaya katika moto huo.

Mamlaka nchini Kenya zinaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo na hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya washukiwa hao.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *