Friday, 28 August 2026

BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA KUKUTANA KWA DHARURA KUJADILI UVAMIZI WA ISRAEL NCHINI LEBANON

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya kikao cha dharura kujadili mashambulizi na uvamizi unaoendelea kufanywa na Israel nchini Lebanon, huku hali ya usalama katika eneo hilo ikiendelea kuzorota. Kikao hicho kimeombwa na Rais wa Emmanuel Macron, ambaye alisema hakuna kinachoweza kuhalalisha operesheni ya kijeshi ya Israel kusini mwa Lebanon. Macron ametoa wito […]

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya kikao cha dharura kujadili mashambulizi na uvamizi unaoendelea kufanywa na Israel nchini Lebanon, huku hali ya usalama katika eneo hilo ikiendelea kuzorota.

Kikao hicho kimeombwa na Rais wa Emmanuel Macron, ambaye alisema hakuna kinachoweza kuhalalisha operesheni ya kijeshi ya Israel kusini mwa Lebanon. Macron ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano ili kuzuia kuongezeka kwa madhara kwa raia.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameahidi kuwa jeshi la nchi hiyo litaendelea kusonga mbele ndani ya Lebanon baada ya kutwaa ngome ya kihistoria ya Beaufort. Netanyahu amesema hatua hiyo ni mafanikio makubwa katika vita dhidi ya Hezbollah.

Mapigano ya sasa yalianza Machi 2 baada ya Hezbollah kujiunga na vita vilivyoanzishwa na Israel na Marekani dhidi ya Iran. Tangu wakati huo, Lebanon imeripoti vifo vya watu 3,412 huku upande wa Israel ukithibitisha vifo vya watu 25.

Jumuiya ya kimataifa imeendelea kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, huku hofu ikiongezeka kuwa mzozo huo unaweza kusababisha hali mbaya zaidi ya kibinadamu katika eneo la Mashariki ya Kati.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *