Saturday, 29 August 2026

MATUMIZI YA BANGI YAONGEZEKA KWA 34% DUNIANI

Waziri wa Nchi, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa matumizi ya bangi duniani yameongezeka kwa 34% katika muongo mmoja uliopita. Amelieleza Bunge Mei 29,206 kuwa Ripoti inaonyesha kuwa takribani watu milioni 244 walitumia bangi mwaka 2023, huku Amerika Kaskazini ikiongoza kwa matumizi hayo duniani. ​“Barani Afrika, maeneo ya Kusini, Magharibi, na Kati yanaongoza kwa matumizi, ambapo […]

Waziri wa Nchi, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa matumizi ya bangi duniani yameongezeka kwa 34% katika muongo mmoja uliopita.

Amelieleza Bunge Mei 29,206 kuwa Ripoti inaonyesha kuwa takribani watu milioni 244 walitumia bangi mwaka 2023, huku Amerika Kaskazini ikiongoza kwa matumizi hayo duniani.

​“Barani Afrika, maeneo ya Kusini, Magharibi, na Kati yanaongoza kwa matumizi, ambapo takribani 10% ya watu wenye umri wa miaka 15 hadi 64 walitumia bangi kwa mwaka mmoja. Aidha, 44% ya bangi yote iliyokamatwa duniani mnamo mwaka 2023 ilitokea barani Afrika,” amesema Prof. Kabudi

Morogoro, Tabora na Mara waongoza kwa kulima bangi nchini
Kamishna Jenerali wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo amesema mikoa ya Morogoro, Mara na Tabora ndiyo vinara wa kilimo cha bangi nchini kwa sasa, hali inayotokana na kuhama kwa maeneo ya uzalishaji kufuatia operesheni mbalimbali zinazotekelezwa na serikali katika mikoa iliyokuwa ikiongoza hapo awali.

Akizungumza Mei 29,2026 na waandishi wa habari bungeni jijini Dodoma, Lyimo amesema hapo awali Mkoa wa Arusha ulikuwa ukitajwa zaidi kwa kilimo hicho, lakini baada ya serikali kuimarisha operesheni za kudhibiti shughuli hizo, uzalishaji ulipungua na hatimaye Morogoro kuchukua nafasi ya juu, ikifuatiwa na Mara na Tabora.

Ameeleza kuwa serikali kupitia Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya imeendelea kuimarisha mikakati ya kupambana na kilimo cha bangi kwa kuongeza doria na operesheni katika maeneo yanayohusishwa na uzalishaji wa dawa hizo, sambamba na kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Katika hatua nyingine, Lyimo amesema Tanzania imepiga hatua katika kudhibiti usambazaji wa dawa za kulevya za viwandani kama heroin, cocaine, methamphetamine na mandrax. Amesema ongezeko la waraibu wanaojitokeza kupata matibabu linaashiria kupungua kwa upatikanaji wa dawa hizo mitaani kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *